Habari ya leo ndugu yangu
uliyeamua kufanya biashara mwaka Huu !
Nikupongeze kuwa umeamua vizuri sana na
matunda yake utayaona mbeleni . Huwezi kuamini kuwa siku ndiyo zinakimbia hivyo .Ushauri wangu ni kuwa ile tabia
uliyokuwa nayo ya kusema nitafanya kesho ,nitafanya mwezi ujao
,nitafanya....naomba uachane nayo kabisa mwaka huu na amua kufanya leo
.Kwanini ufanye leo? ni kwasababu kesho hatuijui na hatujui kama tulivyonavyo na
mawazo tuliyonayo yatafanya kazi kesho .
Siku moja rafiki yangu Hans Mkurugenzi wa HAYATE Organic Farms anayejihusisha na ulimaji wa STRAWBERRY na BLACKBERY
aliniambia kuwa JYB sasa mwaka umeanza ni mwendo wa kukimbizana tofauti na
ilivyokuwa mwaka jana.Nilimpongeza nikasema umeamua vema na matokeo
utayaona badae kabla mwaka haujaisha .
Niachana na hayo nilikuwa
tu najaribu kuamsha akili yako na kukuonesha jinsi gani muda siyo rafiki .Muda
ni sasa anza sasa wala si kesho kama
unavyoweza kuwa unafikiri .
Leo katika hatua ya tatu niliahidi kukueleza
jinsi ya kupata mawazo ya kibiashara .Watu wengi wamekuwa wanalalamika kuwa
hawana mitaji lakini kumbe ukifuatilia shida si mtaji shida ni kwamba hawana
mawazo .Na ukweli ni kuwa msingi wa biashara na mambo makubwa unayoyaona duniani
yakifanyika na yanayoeendelea kufanyika yanatokana na mawazo ya watu .
Mawazo yanafananishwa na
mbegu(seeds) ambazo zikipandwa huzaa mbegu nyingi zaidi .Nilazima uwe na mbegu
za mahindi zipandwe kwenye udongo sahihi ndipo unaweza kupata mahindi mengi
zaidi .Mawazo yako ndiyo yatakufanya kuwa na biashara mwaka huu kwa hiyo
usitafute kwanza mtaji ,tafuta kwanza wazo maana mawazo mengine ni mitaji tosha
kabisa.
Zifuatazo ni njia
zilizodhibitishwa kimataifa za namna ya kupata mawazo mazuri hussusani mawazo
ya biashara .
1. Soma vitabu kila siku(read books)
Ukitaka kupata mawazo mapya
hakuna namna utakwepa kusoma vitabu kila siku na kupata maarifa mapya .Kupitia
vitabu unaweza kupata wazo zuri kupitia maarifa unayopata .Kwenye vitabu yapo
mawazo mazuri ambayo unaweza kukutana nayo na ya kukusaidia .Jambo moja ambalo
nataka niliweke wazi hapa ni kuwa wazo lako si lazima sana liwe jipya .Unaweza
kupata wazo ambalo tayari lipo lakini wewe ukariboresha .
Kama hukuwa mtu wa
kusoma vitabu amua sasa kuanza kusoma vitabu ambavyo ndivyo vyenye mawazo
mengi yanayoweza kukusaidia .Soma vitabu vya ujasiriamali na humu utakutana na
mawazo mazuri .
2.Kuwa mtu wa kuchunguza
vitu (Observe things)
Hii pia ni njia ambayo
inasaidia kupata wazo zuri .unapopata ziara kwenda mahali fulani ni njia nzuri
ya kujifunza na kupata mawazo mapya ,chunguza sana vitu utakavyovikuta huko
.Unaweza kupata wazo kokote kule kama ni mtu unayechunguza vitu .Kuna watu wao
wakisafiri njia nzima wanalala tu ,hawa hawapendi kujifunza na kupata mawazo
kwao si kitu rahisi na chepesi .
Wakati wa sikukuu ya Krismasi ya mwaka 2016 nilipata kwenda Mbeya ambako ndiko wanafamilia tulikuwa tunakutana
.Nikiwa huko niligundua kuwa Mbeya bado haijaamka sana na yapo mengi ambayo bado
hajafanyika na hata kama yanafanyika hayafanyiki kwa ubora na ustadi ...Ni
sehemu ambayo ukikaa unaweza kufanya vitu vingi sana
3. Peruzi Kwenye mitandao
(web surfing) ;
Dunia ya leo ya Teknolojia ya Mawasiliano na
Habari(TEHEMA) imeturahisishia vingi lakini kwa uzembe wetu tumeshindwa kutumia
mtandao vizuri .Tuna simu nzuri sana ambazo kupitia hizo tunaweza kujifunza
mambo mengi lakini simu zetu zimekuwa za kuchat tu watsap na kubadilisha profile zetu facebook..
Siku moja nilikuwa naperuzi
kwenye mtandao wa youtube ,nikakuta video moja ambayo imeonesha mawazo 40 ya
biashara ambayo unaweza kuyafanyia kazi .Nilikaaa chini naa kuanza kuisikiliza
,ukweli ni video nzuri sana na mawazo yote ni mazuri
Acha kuchat tu mpendwa
tumia simu yako kujifunza vitu ...sisemi uache kabisa kuchat lakini tumia muda mwingi
kujifunza .
5. Penda kuandika (Keep
Journal)
Kimsingi huwa tunazalisha
mawazo mengi sana kwa siku lakini hatuna utamaduni wa kuandika mawazo
yanayokuja akilini mwetu .Kuna mawazo tuliyapoteza kwa kutokuandika na
kuyapuzia na hayo watu wengine walivyoyapata wamekuwa matajiri .Mawazo yatakuja
popote na muda wowote kwa hiyo ni muhimu kuwa na journal .Simu yako ya mkononi
inaweza kukusaidia au Diary book .Katika mawazo mengi unayozalisha na
kuyaandika utapata wazo zuri .
6. Tafuta marafiki wapya na
wazuri :
Ni muhimu kuhakikisha kuwa unapata
marafiki wapya kwa namna yoyote .Kuna watu kwa mwezi hawatafuti marafiki
wapya na wamekuwa ni watu wa kukaa na watu wale wale ,wenye tabia na mawazo
yale yale na wamewafanya wasifikirie zaidi ya wanavyofikiri na sasa wanasema
hawana mawazo ya kibiashara .
Ndugu, watu waliofanikiwa na
wanaofanikiwa wana tabia ya kutafuta marafiki wapya ,wenye mawazo mapya
,mitazamo chanya na kiu ya mafanikio.Hakuna namna utapata mawazo mapya na
mazuri kama unakuwa na marafiki wale wale .
Kwa leo tuishie hapa kesho nitakueleza vitu vya kufanya
baada ya kupata wazo zuri la kibiashara ikiwa ni sehemu ya NNE .Usikose kabisa kufuatilia mfululizo huu kama
kweli una nia ya dhati ya kuanza biashara yako kwa mwaka huu.
Joas 0656110906