NITAMILIKI BIASHARA YANGU SEHEMU YA NNE (4) ~Jyb





Baada ya  kueleza namna ya kupata mawazo hussusani mawazo mazuri ya kuanzisha biashara leo nataka nikueleze mambo ya kufanya baada ya kupata mawazo mazuri ya biashara .Mambo haya hayako kwenye mtaala wowote wa darasani hata kama utaenda kusomea Havard .Unapopata mawazo mazuri ya biashara anza kufanya yafuatayo mara moja bila kuchelea :

1.Chuja na Weka vipaumbele vya mawazo yako 
        ( Filter your ideas &Priotize them)

Kuna wakati unaweza kupata mawazo mengi na ukashindwa ufanyie kazi wazo gani .Unapokuwa na wazo zaidi ya moja ni ngumu sana kufanyia kazi mawazo yote kwa wakati mmoja hivyo unapaswa kukaa chini na kuangalia wazo gani unapaswa kuanza nalo kwa kuzingatia uhitaji ,rasilimali ulizo nazo n.k

Watu wengi wameshindwa kuanzisha vitu kwa sababu wanataka waanze na mawazo yote waliyonayo kwa wakati mmoja jambo ambalo hupelekea kushindwa kufanyia kazi wazo lolote .Iko hivi kwamba unapokuwa na wazo zaidi ya moja na unataka kufanyia kazi yote kwa wakati mmoja kinachotokea kinaitwa "ideas conflict " . Hii ni kama vita inayotokea akilini na kupelekea kushindwa kuamua kama hutakuwa makini .

Ni muhimu sana ukamaliza jambo moja (focus on one thing) halafu ndipo jambo lingine lifanyike  kinyume na hapa utakuwa kama fisi aliyetaka yote kwa pupa mwisho akakosa yote .


2.Tafuta Taarifa juu ya wazo lako
      (Find information/Do Research)

Baada ya kupata wazo la kuanza nalo ni muhimu ukaanza kutafuta taarifa sahihi kuhusiana na wazo unalotaka kufanyia kazi .Taarifa hizo ni pamoja na taarifa za washindani wako wanafanyeje ,taarifa za masoko ,taarifa juu ya changamoto na hatari zinazoweza kutokea kama utaweza  kufanyia kazii wazo lako .

Taarifa hutoa picha (blue print) ya namna wazo lako linavyoweza kufanikiwa au kushindwa .Hii ni muhimu sana lakini kwa bahati mbaya watu wengi wameshindwa kuendelea au kuanzisha biashara kwa sababu hawana taarifa au wana taarifa ambazo si sahihi kuhusiana na kile wanachoweza kufanya .

Angalizo ni kuwa usimtume mtu akutafutie taarifa ,tafuta mwenyewe taarifa  maana taarifa ya kuletewa huwa inadanganya .


3.Tafuta Maarifa ( Seek Knowledge)
Ugonjwa mkubwa wa watu wengi Hussusani watanzania ni kwamba hawataki kutafuta maarifa na kukuza ufahamu wao .Ni watu wanafanya vitu kienyeji .Hawataji kujifunza lakini wanataka matokeo makubwa wakati hawana maarifa.

Mwaka  huu  unapowaza kumiliki biashara yako waza kutafuta maarifa .Maarifa ndiyo nguvu yako ,maarifa ndiyo yatakufanya ufanye tofauti na wengine .Maarifa ndiyo yatakufanya uendelee hata kama mazingira ni magumu .

Azimia kuanza kusoma vitabu na kufuatilia kwa upana kile unachowaza kufanya .Hudhuria semina mbalimbali hata kama ni za kulipia .Jiunge na makundi ya watsap na Telegram mazuri yanayoongeza vitu kila siku achana na makundi yanayongelea habari za michezo ,udaku ,umbeya na matukio ya watu .Anza kufuatilia vitu kwenye mtandao kupitia simu yako na utaona badiliko na matokeo makubwa  .


Joas 0656110906 (Jyb)