Baada
ya kuwa umepata wazo la biashara kuna mambo kadhaa unapaswa kufanya kuelekea
kumiliki biashara yako.Mambo hayo watu wengi wamekuwa hawafanyi kabisa na hii imesababisha kutoanza
biashara au biashara kutopiga hatua kubwa
.Vitu vya kufanya baada ya kuwa umepata wazo ni pamoja na :
1.Andaa mchanganuo wa
kibiashara (business plan)
Inashauriwa
kuwa kabla ya kufanya biashara uandae mchanganuo wa biashara yako ili kujua
unahitaji mtaji wa kuanzia kiasi gani ,wateja unaowalenga ni watu gani
,washindani wako ni watu gani n.k .Mchanganuo huu ndio hata taasisi na watu
wanaoweza kukusaidia na kuwezesha wazo lako huwa wanahitaji .
Wito
wangu ni kuwa tuache kufanya mambo kienyeji
ill tuboreshe na tupige hatua katika biashara zetu na watu washangae .Mtu
mwingine naona anaanza kujiuliza kuwa " hivi hata biashara yangu ndogo
nayowaza nitahitaji mchanganuo wa biashara???" Jibu ni ndiyo .Kila kiashara inahitaji kuwa
na mchanganuo wake ili iwe yenye tija.
Kwa
bahati nzuri rafiki yangu Lendian Bigoli
0788603066 ni mtaalamu wa kutengeneza mchanganuo wa biashara unaweza kumtafuta
kwa njia ya simu akakusaidia ...Bei zake ni msaada kabisa tosha kwako wewe
uliyeamua kuanzisha biashara .
Kupitia
mtandao pia unaweza pia kupakua (download) mifano ya mchanganuo wa biashara
ukaanza kuandaa mchanganuo wako lakini nakushauri uwasiliane na wataalam
wakusaidie .
2. Andaa mpango wa kimasoko
(Marketing plan)
Ni muhimu sana wakati hujaanza kuingia kwenye biashara hili nalo ukaanza
kulifikiri .Biashara nyingi nimeshuhudia zikifa kwa kukosa wateja kwa sababu
wakati zinaanza hakukuwepo na mchango wowote wa kimasoko.
Baada
ya kuandaa mpango wa biashara kaa chini tengeneza mpango wa kimasoko ili ujue
unaingia na mbinu gani katika soko hata kama washindani ni wengi .Ndiyo ,
acha kufanya mambo kimazoea amua kubadilika na kufanya mambo kwa utofauti na
kwa waredi .
Kama
hujui namna ya kuandika rafiki yangu Franklin 0766 133 413 ni mtaalamu mwenye
shahada ya kwanza katika masoko na amefanya kazi nyingi .Pata muda umtafute na
akuelekeze hata kwa njia ya mtandao namna ya kuandika mpango wa kimasoko.
3.Tafuta mtaji
Baada
ya kuandika mpango wa biashara na masoko ni muda muafaka wa kutafuta mtaji wa kibiashara
.Angalizo Hata kama utapata fedha za mtaji bila kuwa na mipango inayoeleweka
hela yako haitaonekana na inaweza kupotea kabisa ukashangaa.Kupata mtaji sehemu
yenye mipango ni jambo rahisi kabisa
kulio kupata mtaji sehemu ambayo unachotaka kufanya hakielewiki
kimaandishi .
Joas 0656110906
Habari Njema kwako juu ya
Uandishi wa Mpango wa biashara
Siku
ya Jumamos tarehe 3/6/2017 pale Jengo la City Furniture lililoko Kariakoo
darajani (Gerezani) Jirani na Mkuki House ghorofa ya tatu chumba namba 309
, JOINT PROFFESSIONALS CO. LTD Kwa
kushirikiana na JYB pamoja na VIPAWA LINK ASSOCIATIONS wamekuandalia mafunzo ya
namna ya kuandika mchanganuo /mpango wa biashara kwako wewe .
Hii
ni nafasi adhimu kwako wewe mjasiriamali na mafunzo haya siyo ya kupuuza kwani
yamekuwa hayafundishwi kokote hata mwalimu wako wa biashara anaweza kuwa
hakukueleza vizuri kuhusu hili .
Lazima
ufahamu kuwa uandishi wa mchanganuo wa biashara ni gharama sana lakini siku
hiyo utajifunza kwa gharama ya sh 10,000/= tu na mara baada ya hapo utakuwa na
uwezo wa kuandika na utaweza pia kuanza kuwaandikia wengine na ikawa sehemu
yako ya kujipatia kipatao .Hii siyo ya Kupuuza .
Tutakuwa
na mtaalamu aliyebobea katika uandishi wa wa mpango wa biashara na miradi ndugu
Lendian Bigoli Mkurungezi wa Sound Mind Consultants ambaye ameandika miradi mingi sana na mpaka sasa .Njoo upate
maarifa .
Nafasi
zipo arobaini tu (40) Hivyo tuma mchango
wako kujiandikisha kupitia namba hizi
0657267074 /0744630713 /0656110906 .Nafasi hizi ni chache changamkia
fursa hii adhimu bila kuchelea maana waswahili husema "mchelea mwana kulia
hulia yeye"