![]() |
Mwandishi wa kitabu cha INUKA |
Habari
yako?, naitwa Kashindi
Edson, nimejitokeza katika kitabu hiki cha INUKA kuzungumza machache
niliyojaliwa kufahamu juu ya mwandishi wa hiki kitabu ulichoshika mkononi
mwako. Kwanza kabisa natanguliza shukrani za dhati kutoka kwenye sakafu ya moyo
wangu kwa ndugu Joas, mshauri wangu kwa kunipa fursa hii adhimu inayoandika
historia mpya kabisa katika maisha yangu na familia yangu, nashukuru sana kwa
heshima hii kubwa aliyonipa na kuamini katika huu mchango wangu mdogo kwenye
uandishi wa kitabu cha INUKA. Kitabu kilichobadili na kinachoendelea kubadilia
maelfu ya watanzania kwa kasi ya ajabu sana. INUKA ni kitabu kilichobeba nguvu
kubwa na siri ambazo hazikuwahi kuzungumziwa mahali popote kwa muda wa miaka
mingi. Ni bahati kubwa sana kupata fursa ya kusoma hiki kitabu.
Sijui upo unasoma kitabu hiki kwa malengo gani, lakini naamini kuna kitu unakitaka katika maisha yako. Naamini una kiu na shauku ya kubadilisha maisha yako kutoka hapo ulipo leo kwenda kule unakotaka kwenda. INUKA, ni kitabu kinachorithi na kuendeleza busara, mawazo, mbinu na siri za watu waliokwisha INUKA NA KUFANIKIWA katika maeneo karibu yote. Joas analenga kukuinua na kukutoa hapo ulipo wewe mwenye ndoto kubwa ya kuwa mfanyabiashara, mjasiriamali, kiongozi, mhamasishaji, mwandishi, msomi, mwanamichezo na mwekezaji mkubwa.
Tunapokuja katika mafanikio ya kiuchumi(kipesa),
huwa bwana Joas haamini hata kwa asilimia moja kama kuna mtua anaweza kuwa na
uhuru wa kifedha katika AJIRA. Miaka michache nyuma, Joas amewahi kuwa
mwajiriwa waTaasisi ya fedha(Microfinance)
Platinum Credit iliyoko nchini Tanzania ,Kenya ,Uganda na Afrika Kusini.
Alifanya kazi kwa muda karibu wa mwaka mmoja kabla ya kuacha kazi kwa masikitiko
na majonzi makubwa sana na kujutia kupoteza muda huku akidai kuwa kwenye ajira
hakuna baadaye iliyo bora (there is no
better future in employment). Kidogo ni jambo la kushangaza.
Siku moja niliwahi kumuuliza hivi, “Kaka unajua
jinsi watu wanavyohangaika kutafuta ajira bila mafanikio?”. Majibu yake yakawa
kama ifuatavyo, “Dogo nachohitaji ni kuwa huru na kufanya mambo yangu na kuwa karibu na
watu naohitaji kuwa karibu nao. Ningekuwa bado kwenye ajira hata wewe leo hii
usingeweza kuwa karibu yangu. Kwenye ajira hakuna uhuru kabisa wa kutumia uwezo
ambao Mungu ametupa bure. Siwezi kufanya kazi ya mtu tena”.
![]() |
Lilian akiwa na kitabu tayari |
Kuonesha kuwa Joas haamini kuwa ajira pekee ndiyo
itamfanikisha mtu, baada tu ya kuacha kazi katika taasisi ya Platinum Credit alianzisha (movement) vuguvugu
la kuwafundisha vijana ujasiriamali, jinsi ya kugundua na kutumia vipaji vyao
na mbinu za kisasa za biashara inayenda kwa jina la Youth Transformation and Development Program (YTDP) Ni miongoni mwa
PROGRAMU za kijamii zinazoleta
mabadiliko ya kifikra kwa vijana hapa nchini. Baadaye kidogo tutaiongelea kwa
undani zaidi.
Joas ni mtu wa namna yake. Siku ya
uzinduzi wa hiki kitabu, Kaka yake bwana Eliphas Buyungu alisema kwamba “Sio
haya tu kuna vitu vingi ambavyo hamvifahamu, kuna mambo ambayo huwa Joas
anayafanya mpaka tunashindwa kuelewa hivi ni yeye au ni mwingine?”.
Ushindi Elioth (ntamuongelea baadaye kidogo) alisema hivi, “kipindi tuko shule Joas
alikuwa mpole sana”. Kelvin
Kitaso, aliwahi kuniambia kwamba, kipindi wako Chuo, Joas alikuwa mpole sana
lakini mpaka sasa ni miongoni mwa vijana wachache sana wanaojitahidi
kubadilisha maisha ya watu kwa kiwango cha juu sana.
Binafsi, Joas ametoa mchango mkubwa sana katika
maisha yangu, siyo tu katika kuendeleza kipaji changu cha uandishi, pia ameweza
kuniunganisha na kunikutanisha na watu ambao najivunia sana kuwafahamu na kuwa
nao leo katika maisha yangu. Sitoacha kushukuru na nitaendelea kushukuru mara
kwa mara. Bila yeye, leo nisingekuwa namfahamu Kelvin Kitaso, bila yeye
nisingekuwa nikimfahamu Adabert Chenche, bila yeye nisingeweza kukutana wala
kumfahamu Elioth Ushindi, na wengine wengi ambao kwa sehemu kubwa wameathiri
maisha yangu na kunijenga kimaono zaidi.
JOAS ni kijana mhamasishaji,
mwandishi na mfanyabiasha wa kitanzania anayefamika zaidi kwa jina la Jyb. Jyb ni kifupisho cha majina yake
matatu; JOAS YUNUS BUYUNGU pia ni kifupi cha jina la kampuni yake maarufu ya
ubunifu na ushonaji wa nguo na graphics design inayoenda kwa jina la JYB Modern Company aliyoianzisha na
kuiasisi mwaka 2015 jijini Dar es salaam.
Joas
ameweza kufahamika na kupata umaarufu kupitia mitandao ya kijamii kama vile
facebook, twitter, instagram, skype na whatsup na blogs mbalimbali za kiswahili
kama www.kijanajithamini1.blogspot.com, www.maishanamafanikio.blogspot.com. Jina la Joas linazidi kujulikana na kuwa
maarufu sio tu Tanzania, bali Afrika Mashariki na kati kwa sababu ya uwezo wake
mkubwa wa kugusa, kuhamasisha na kubadilisha maisha ya watu wengi hasa vijana
katika maeneo ya uongozi, biashara, imani, ujasiriamali na saikolojia.
JOAS, WAZAZI NA NDUGU ZAKE.
![]() |
Jackson Silvery akiwa na kitabu cha Inuka |
Siku moja nimewahi kumuuliza Joas kwanini anabidii
sana na hulka ya kufanya kazi kwa bidii? Katika maswali ambayo nimewahi
kumuuliza hili ni swali ambalo lilionekana kumfurahisha, alicheka kidogo kisha
akasema hivi, “Mama yangu alikuwa ni mtu wa mwisho kulala pia alikuwa ni wa kwanza
kuamka. Kwa hiyo mama yangu alinifundisha kujituma sana na kuongeza bidii kila
siku kwa kile ninachokifanya. Anaendelea kusema, siku zote tumekuwa tukiwapa
nafasi sana baba zetu kwa sababu ni wanaume, ila kwangu mimi ni tofauti, mama
alikuwa akinivutia sana, alijituma sana na mimi najituma sana kwa sababu ni
kitu ambacho nilijifunza kwa mama yangu.
Kumbuka kuwa, Joas ni
mtoto wa tatu kutoka mwisho, ana ndugu tisa na mpaka leo amempoteza dada yake
mmoja ambaye alishatengulia mbele ya haki na mimi natumia fursa hii kumuombea
kwa Mungu, alale mahali pema peponi amina!. Joas ni miongoni mwa watu
waliobahatika kuzaliwa katika familia kubwa, yenye watoto wengi. Nakumbuka siku
ya uzinduzi wa hiki kitabu, nilikuwa nimekaa kiti cha kwanza mbele kabisa,
nilikuwa na rafiki yangu Francis, nilishangaa kusikia Francis akiniambia hivi, “Edson,
Joas ana ndugu wengi, halafu
wanaoonekana wanajaliana!”. Hapo ilikuwa ni wakati wa kufungua kitabu
ambapo kila mtu alipewa kipaza sauti na kujitambulisha na kununua kitabu.
Kama nilivyokwisha sema, Joas anazaliwa katika
familia ya watoto kumi yeye akiwa ni mtoto wa nane kuzaliwa, tukimuondoa huyu
ambaye alishatangulia mbele za haki, kuna Elias Yunus ambaye ni kitinda mimba,
kuna Elianson Yunus, Devotha Yunus, Grace Yunus, Jackson Yunus, Anastastina
Yunus, Elihud Yunus na Eric Yunus ambaye ni kifungua mimba.Na asilimia tisini
ya hawa ndugu wote wa Joas wamesoma na ni wafanyakazi wengine wamejiajiri. Kwa
kifupi Joas anatoka katika famila iliyo na mafanikio makubwa kielimu, kiimani na kijamii pia.
Mafanikio ya Joas kiroho, kifikra na kijamii ni picha halisi ya familia yake.
WALIMU NA ELIMU YAKE.
KITAALUMA, Joas ni mwanasayansi wa sayansi ya kompyuta. Amehitimu shahada ya sayansi ya kompyuta mwaka 2014 katika chuo kikuu cha Dar es salaamu. Akiwa Chuo aliweza kukutana na rafiki yake kipenzi bwana Kelvin Kitaso(ntamuongelea baadaye kidogo) pia maisha yake ya chuo yalikuwa ya kiimani sana na alipendelea kuwa katika vikundi vya dini. Huyu rafiki yake alikuwa kiongozi wa Casfeta Tayomi, kikundi cha dini kabla ya kuwa mchungaji msaidizi. Wakati huo Kelvin Kitaso alikuwa ni mwandishi tayari. Mbali na Kelvin Kitaso kuna kijana mwingine anayeenda kwa jina la Adabert Chenche, mwandishi wa vitabu kama vile Kwanini Ufeli? n.k.
![]() |
Dada Magreth akiwa amejipatia kitabu cha Inuka |
Kidato cha tano na cha sita, Joas alikuwa akisoma
mchepuo wa PCM, Physics, Chemistry na
Mathematics. Embu chukua sekunde thelathini kutafakari aina ya watu
wanaochukua michepuo kama hii ya Joas, bila shaka utagundua ni watu wenye uwezo
mkubwa sana darasani. Elimu yake ya kidato cha tano na cha sita aliichukua
katika shule maarufu sana hapa Dar es salaamu, Pugu Sekondari School.Maisha
yake hapo shuleni Pugu alimpenda sana Mwalimu Manyilizu. Alikuwa ni mwalimu
wake wa Hesabu. Kidato cha kwanza na cha pili alisoma shule ya Kantalamba
iliyoko Sumbawanga na alikuwa mwanafaunzi aliyependa kuwafundisha wanafunzi
wenzake. Hakuwahi kuwa mbinafsi maisha yake yote. Wanafunzi wenzake walimpenda
kwa sababu ya moyo wake wa kuwasaidia wenzake. Joas hajabadilika, mpaka leo ni
mtu wa kujitahidi kuisaidia jamii kutoka hapo ilipo kwenda pale inapotamani
kuwa.
KWA upande wangu mimi, maisha yangu yote tangu
nimefahamu kusoma na kuandika, nimekuwa msomaji wa vitabu vya aina zote.
Sijisifii ila nilijua kuandika jina langu siku ya kwanza nilipoenda shule, hata
kabla sijaanza shule nilipenda kalamu na karatas kuliko hata chakula. Nimeanza
kusoma vitabu ambavyo siyo vya kujibia mtihani tangu niko vidudu, nimeanza
kusoma hadithi za kwenye magazeti tangu mdogo sana. Namshukuru sana Mwalimu
wangu tangu mtoto, Mwalimu Weston Yohana, maarufu kama Tesa. Alitambua kuwa
nilikuwa napenda vitabu kwa hiyo muda wote alikuwa akinipa vitabu. Kwa muda wa
miaka mingi, waandishi wengi wamekuwa wakimwambia msomaji wao kuwa INAWEZEKANA
lakini hawasemi INAWEZEKANA VIPI.
Joas sio mtu wa kukuambia kuwa
inawezekana tu, bali pia ni mtu wa kukuambia inawezekana vipi. Siku zote
amekuwa sio mhamasishaji tu bali ni mwalimu na mkufunzi wa mafanikio anayetoa
njia na mbinu zilizo rahisi kufikia ndoto na malengo yako. Kama umewahi kukaa
na Joas au hata kuzungumza naye utakuwa ni shahidi wa hili ambalo nataka
niliseme, Joas ni mzuri sana katika kuzungumza Kiigereza. Hatusemi kwamba kujua
au kutokujua kingereza ni maada ya kujadiliana, hapana!, hata kama ni mada ya
kujadiliana, kwani hatujui kuwa Tanzania ni nchi inayoongoza kuwa na wahitimu
wasioweza hata kujieleza kwa kingereza?. Tuachane na hayo. Nachomaanisha hapa
ni kwamba, Joas hakusoma mchepuo wa Kiingereza wala Historia, mara nyingi
tunaamini kuwa wanafunzi wa masomo ya sanaa huwa ndiyo wazuri katika kuongea
kiingereza na huo ndio ukweli na mimi ninayeongea hivi kitaaluma ni Mwalimu kwa
hiyo na tajiriba ya kutosha katika hili eneo.
NILIWAHI kumuuliza, Joas, ulijifunza lini na wapi
kuzungumza Kiingereza fasaha kiasa hicho?. “Mwalimu wangu wa shule ya msingi alikuwa
vizuri sana. Alikuwa akitufundisha kwa namna ambayo lazima utajua pia utaelewa.
Nilikuwa nikimpenda sana Mwalimu wangu wa kiingereza, Mwalimu Ezekiel Marius
alijua sana kufundisha kingereza kwa ustadi mkubwa.”
MARAFIKI NA WAHAMASISHAJI WA JOAS
ZIG ZIGLAR, aliwahi kusema hivi, “ukiwa karibu ya
watu watano wanaojiamini jiandae kuwa mtu wa sita kujiamini, ukiwa karibu ya
watu watano wenye busara, jiandae kuwa mtu wa sita kwa busara, ukiwa karibu ya
watu watano wenye pesa jiandae kuwa mtu wa sita kwa pesa na ukiwa karibu ya
wapumbavu watano jiandae kuwa………………… Kwa lugha nyingine tunasema hivi, sisi ni
wastani wa watu sita tulioishi na kukaa
nao kwa kipindi kirefu cha maisha yetu. Waganda wanasema hivi, “nioneshe rafiki zako nitakuambia wewe ni
nani”(show me your friends, I shall tell you who you are).

ILIKUWA
ni mwanzoni mwa mwaka wa 2016, ambapo Joas alinipigia simu na kuniambia kwamba
kuna mtu anaitwa Kelvin Kitaso anahitaji mtu wa kumsambazia vitabu na
kunielekeza kuwa kwa kila kitabu unachouza kuna asilimia fulani kwa ajili yako.
Nilifurahi sana na baadaye kidogo Kelvin Kitaso alinipigia simu na kuniambia
kuwa namba yangu alipewa na bwana Joas na kunieleza kila kitu na tukapanga siku
ya kuonana huku tukikubaliana kwamba atakuja DUCE(Chuo nilichokuwa nasoma kipindi hicho) na vitabu ili niwe
naviuza chuoni na sehemu zingine. Nakumbuka alikuja siku ya jumapili akiwa
ameambatana na binti fulani ambaye sikuwa nikimfahamu, tuliongea ingawa sio kwa
muda mrefu ila alionekana kusikitishwa na vijana kutosoma vitabu vya maendeleo
binafsi. Kabla ya hapo nilianza kumsikia Kelvin Kitaso kupitia kundi la KIJANA JITHAMINI.
JOAS nimemfahamu muda mrefu sana,
zaidi ya miaka kumi, Joas hakuwa mwandishi zaidi tu, Joas alipenda kusoma
vitabu. Kuna kipindi nilipotezana naye nikawa siwasiliani naye kwa kipindi cha
zaidi ya miaka mitatu na nadhani ilikuwa ni kwa sababu ya shule. Mimi nimeanza
kuandika makala za hip hop, falsafa na masuala ya harakati facebook. Kuna siku
nilibahatika kumuona Joas facebook ikabidi nimuombe urafiki. Nilianza kuona
akiandika masuala ya kufikirisha na yenye changamoto huku akitumia falsafa za
akina Jim Rohn na Kop Meyer. Sikushangaa sana kwa sababu
Joas alisoma sana vitabu tangu zamani. Baadaye kidogo nikaanza kutoa maoni na
kumuuliza maswali ya yaliyobeba changamoto za makala zake. Hazikupita siku
nyingi Joas alinitumia ujumbe na tukaanza kuwasiliana tena na kurudisha ukaribu
wetu kama ilivyokuwa zamani.
Aliniuliza malengo yangu nini nikamuambia.
Nachoshukuru tu Joas anapenda sana watu wafanikiwe na nadhani hii ndiyo asili
yake.
Hazikupita siku nyingi Joas aliniunganisha kwenye
group la KIJANA JITHAMINI ambapo nilikuja kuanza kuwasikia akina Adabert Chenche,
Ushindi Elioth na wengine wengi ambao ni waandishi. Joas alianza kunichukulia
kama mwandishi, nadhani ni baada ya kujua maono na ndoto zangu, pia kipindi
tunarudisha mawasiliano nilikuwa naandika kitabu kinachohusu masuala ya hip hop
ila kwa bahati mbaya hakijatoka mpaka leo ila tunaamini kitatoka. Mungu
atatusaidia.
BAADA ya muda mfupi tulipata wazo la kuanzisha
magazine(Kijigazeti) la masuala ya uhamasishaji na nakumbuka hilo wazo
lilitufanya kukutana wote mimi, Mihayo, Joas, Kitaso, Adabert na Laban . Kwa
mara ya kwanza nikakutana na Adabert, Mihayo na wengine. Hawa wote kwa pamoja ni
waandishi, jiulize Joas angekuwa nani?. Lazima
Joas angekuwa mwandishi. Kwa hiyo Joas alijikuta yuko katikati ya waandishi
akajikuta na yeye amekuwa mwandishi ukijumlisha na tabia yake ya kusoma vitabu.
JOAS
ni kijana anayepambana usiku na mchana kuathiri kizazi cha sasa na cha kesho na
kuleta matokeo makubwa yaliyo CHANYA katika maisha ya watu wengi zaidi hasa
vijana. Kitaaluma Joas ni mwanasayansi
wa sayansi ya kompyuta, mwasisi wa kundi la kundi la KIJANA JITHAMINI, kundi linaloendesha
shughuli zake kupitia mitandao kama whatsApp, facebook na blogs.
Kijana
Jithamini ni kundi la vijana walioamua kutumia muda wao kuelimishana,
kuhamasishana na kushirikiana katika shughuli mbalimbali za maendeleo na mafanikio.
Vijana wanaounda Kijana Jithamini wamekuwa mfano bora na hamasa kubwa sana kwa
vijana wengi wa kitanzania hasa kwa maono na mitazamo na ndoto kubwa zilizomo
vichwani na mioyoni mwao. Kundi la Kijana Jithamini linaundwa na vijana
walioamua kuacha kulalamika na kuchukua hatua
madhubuti za kupambana na kupiga vita ujinga, maradhi na umaskini nchini
Tanzania na Afrika kwa ujumla.
Miongoni mwa vijana maarufu wanounda kundi hilo
ni; Mwandishi wa kitabu bora cha wanafunzi vyuoni cha Getting Prepared For Post University Life ambaye pia ni Mwasisi na Rais
wa taaisi ya kijamii ya RFGM na Mkurugenzi wa kampuni kubwa ya uchapishaji wa
vitabu hapa nchini Gracious Printing Press, mhamasishaji ndugu Kelvin Kitaso. Adabert Cheche,
mwanzilishi wa taaisi ya VIPAWA LINK, mhamasishaji na mwandishi wa vitabu kama
Kwanini Ufeli, Manukato ya Mafanikio. Ushindi Elioth Mwandishi wa kitabu cha “A walk to financial Freedom “ na Kitabu cha “Urejesho wa Ibada ya Mugu wa kweli”.

Joas pia ni mwandishi wa makala
maarufu sana ya kuhamasisha na kubadalili mitazamo ya haiwezekani kuwa
inawezekana, MORNING RISE UP. Haya
ni makala yanayoandikwa kupitia mitandao ya kijamii na kugusa maisha ya watu
wengi hasa kwa ujumbe muhimu na hamasa kubwa inayobebwa kwenye haya makala.
JOAS, ni watu gani ambao
wamekuhamasisha na kukufanya ufikie hatua ya kuanza kufundisha na kuhamasisha
watu wengine?. “Ni watu wengi. Kwanza kabisa, nahamasishwa na marafiki zangu, akina
Kelvin Kitaso, Adabert Chenche, Daniel Rwihula,Widom Misana ,Adam Ngamange
,Nicholous Mwakyonde(Zingo) , Patrick Roman ,Amina Sanga ,Subira Mlaga ,Rehema
Robert , Fred Mwahelende ,Robson Sisyan ,Seth Jacob, Ushindi Elioth , Lendian
Bigoli ,Jacob Mushi(mwandishi wa kitabu cha Siri saba za kuwa hai Leo), lazaRo
Samwel(mwandishi wa kitabu cha Siri Tatu za Maisha) na wengine wengi. Pia kuna
watu kama Jim Rohn, Robert Kiyosaki, Eric Shigongo, Dr Moyles, na Nelson
Mandela, Napoleon. Najifunza vitu vingi sana kutokwa kwa hawa watu.
HISTORIA ya Joas bado ni ndefu sana na inaishi na
bado inakua. Inapendeza sana kusoma historia huku na wewe ukiwa unaweka
historia.
Usihitaji
kukubalika, hitaji kukumbukwa.
Ahsante
sana. Naitwa Kashindi Edson hongera kwa kupata nakala ya INUKA