KILICHOTUKOSESHA YULE SWALA NI HIKI HAPA...~Jyb






Siku moja tulikuwa tunawinda mimi na rafiki yangu Alex.Wakati tuko tunawinda na mbwa wa jirani maarufu kwa jina la chui ,mbwa alimkurupua swala akiwa amejilaza mahali .Swala alikimbia mbio  na mbwa wetu akakimbia sana akiwa anamkimbiza Swala huyo .Sisi tukawa nyuma tukijua tulikuwa tumepata kitoweo siku hiyo maana mbwa alikuwa anakaribia kumkamata yule Swala .

Wakati mbwa akiwa anakimbizana na swala tulikutana na mto mkubwa ,Swala akaruka mto na mbwa akaruka lakini sisi tukashindwa kuruka .Mbwa alivyoona hatumfuatilii ukawa mwisho akarudi tukawa tumemkosa swala kwa kuwa tulikosa DARAJA la kuvukia ule mto.

Maisha yetu yanahitaji daraja ili tufike kule tunapotaka kufika .Bila kuwa na daraja hutaweza kuvuka ndugu mbio zako zitaishia kwenye kingo za mto .

Nakumbuka habari ya wana wa Israel waliokuwa wakitoka Misri kwenye nchi ya utumwa kwenda Kanani nchi ya Maziwa na asali waliyokuwa wameahidiwa walipokutana na Bahari ya Shamu hawakuendelea mpaka hapo njia mbdala ilipoletwa na Mungu mwenyewe.Mungu alifanyika kuwa daraja la Wana wa Israel.

Ndiyo,Hautatoka hapo ulipo kama hutapata daraja la kukuvusha kule unakotaka kwenda .Unahitaji sasa kujiunga na KUNDI LA WHATSSAP LA DARAJA LA MAISHA ujifunze daraja ambalo litakuvusha kwenda ng'ambo.

Ng'ambo yako ni ndoto ambayo unataka siku moja itimie ,ng'ambo yako ni yale maisha unayotaka kuishi kesho .Hautaweza kuyafikia kama hutapata daraja la kukupeleka kule unakotoka kufika .

Joas(Jyb) ameanzisha kundi mahususi kwa ajili yako ili akupe daraja litakalokuvusha kwenda ng'ambo na pia kwa kujiunga na kundi hili utajipatia nakala ya kitabu cha INUKA TOLEO LA PILI(Harcopy) kitakachotumwa kokote ulipo kuanzia tarehe 26.9.2017 siku ya kuzaliwa kwangu ikiwa ni zawadi nitakayokupa kwako.Mbali na hayo kila siku nakuwa natuma vitabu vya waandishi mbalimbali vifanyike daraja kwako.

Kujiunga na kundi hili unapaswa kulipa kiasi cha shillingi elfu kumi kwa namba zangu hizi

1.0656110906(Tigo Pesa) Joas
2.0753836463(Mpesa) Jina Joas

Kwa kulipa kiingilio hicho utakuwa umekata tiketi ya kujiunga na kundi hilo la kudumu la DALAJA LA MAISHA .Zipo nafasi mia moja tu na mwisho wa kufanya malipo ni tarehe 15.8.2017 baada ya hapo haitapokelewa hela yoyote.

Watu wengi wameonesha mwitikio mkubwa kujiunga na kundi hili ambalo litaleta mageuzi makubwa na kutengeneza waty wenye uwezo wa kutenda.


Acha kufikiria ukubwa au udogo wa elfu kumi angalia matokeo makubwa yatakayoletwa na elfu Kumi kama utajiunga na Kundi la DARAJA LA MAISHA


Joas 0656110906/0753836463


"TUJIUNGE NA DARAJA LA MAISHA TUINUKE WOTE"

WATU WANAMSEMAJE MWANDISHI WA KITABU CHA INUKA ?



Mwandishi wa kitabu cha INUKA
Habari yako?, naitwa Kashindi Edson, nimejitokeza katika kitabu hiki cha INUKA kuzungumza machache niliyojaliwa kufahamu juu ya mwandishi wa hiki kitabu ulichoshika mkononi mwako. Kwanza kabisa natanguliza shukrani za dhati kutoka kwenye sakafu ya moyo wangu kwa ndugu Joas, mshauri wangu kwa kunipa fursa hii adhimu inayoandika historia mpya kabisa katika maisha yangu na familia yangu, nashukuru sana kwa heshima hii kubwa aliyonipa na kuamini katika huu mchango wangu mdogo kwenye uandishi wa kitabu cha INUKA. Kitabu kilichobadili na kinachoendelea kubadilia maelfu ya watanzania kwa kasi ya ajabu sana. INUKA ni kitabu kilichobeba nguvu kubwa na siri ambazo hazikuwahi kuzungumziwa mahali popote kwa muda wa miaka mingi. Ni bahati kubwa sana kupata fursa ya kusoma hiki kitabu.


Sijui upo unasoma kitabu hiki kwa malengo gani, lakini naamini kuna kitu unakitaka katika maisha yako. Naamini una kiu na shauku ya kubadilisha maisha yako kutoka hapo ulipo leo kwenda kule unakotaka kwenda. INUKA, ni kitabu kinachorithi na kuendeleza busara, mawazo, mbinu na siri za watu waliokwisha INUKA NA KUFANIKIWA katika maeneo karibu yote. Joas analenga kukuinua na kukutoa hapo ulipo wewe mwenye ndoto kubwa ya kuwa mfanyabiashara, mjasiriamali, kiongozi, mhamasishaji, mwandishi, msomi, mwanamichezo na mwekezaji mkubwa.
Tunapokuja katika mafanikio ya kiuchumi(kipesa), huwa bwana Joas haamini hata kwa asilimia moja kama kuna mtua anaweza kuwa na uhuru wa kifedha katika AJIRA. Miaka michache nyuma, Joas amewahi kuwa mwajiriwa waTaasisi  ya fedha(Microfinance) Platinum Credit iliyoko nchini Tanzania ,Kenya ,Uganda na Afrika Kusini. Alifanya kazi kwa muda karibu wa mwaka mmoja kabla ya kuacha kazi kwa masikitiko na majonzi makubwa sana na kujutia kupoteza muda huku akidai kuwa kwenye ajira hakuna baadaye iliyo bora (there is no better future in employment). Kidogo ni jambo la kushangaza.
Siku moja niliwahi kumuuliza hivi, “Kaka unajua jinsi watu wanavyohangaika kutafuta ajira bila mafanikio?”. Majibu yake yakawa kama ifuatavyo, “Dogo nachohitaji ni kuwa huru na kufanya mambo yangu na kuwa karibu na watu naohitaji kuwa karibu nao. Ningekuwa bado kwenye ajira hata wewe leo hii usingeweza kuwa karibu yangu. Kwenye ajira hakuna uhuru kabisa wa kutumia uwezo ambao Mungu ametupa bure. Siwezi kufanya kazi ya mtu tena”.
Lilian akiwa na kitabu tayari
Siku hiyo sikurudia kuzungumzia hilo swala tena. Joas anaamini kuwa, “ili mtu aweze kufikia mafanikio ya kifedha hana budi kutumia vipaji ,vipawa na  karama alivyojaliwa na Mwenyezi Mungu”.

Kuonesha kuwa Joas haamini kuwa ajira pekee ndiyo itamfanikisha mtu, baada tu ya kuacha kazi katika taasisi ya Platinum Credit alianzisha (movement) vuguvugu la kuwafundisha vijana ujasiriamali, jinsi ya kugundua na kutumia vipaji vyao na mbinu za kisasa za biashara inayenda kwa jina la Youth Transformation and Development Program (YTDP) Ni miongoni mwa PROGRAMU za kijamii zinazoleta mabadiliko ya kifikra kwa vijana hapa nchini. Baadaye kidogo tutaiongelea kwa undani zaidi.
Joas ni mtu wa namna yake. Siku ya uzinduzi wa hiki kitabu, Kaka yake bwana Eliphas Buyungu alisema kwamba “Sio haya tu kuna vitu vingi ambavyo hamvifahamu, kuna mambo ambayo huwa Joas anayafanya mpaka tunashindwa kuelewa hivi ni yeye au ni mwingine?”. Ushindi Elioth (ntamuongelea baadaye kidogo) alisema hivi, “kipindi tuko shule Joas alikuwa mpole sana.  Kelvin Kitaso, aliwahi kuniambia kwamba, kipindi wako Chuo, Joas alikuwa mpole sana lakini mpaka sasa ni miongoni mwa vijana wachache sana wanaojitahidi kubadilisha maisha ya watu kwa kiwango cha juu sana

Binafsi, Joas ametoa mchango mkubwa sana katika maisha yangu, siyo tu katika kuendeleza kipaji changu cha uandishi, pia ameweza kuniunganisha na kunikutanisha na watu ambao najivunia sana kuwafahamu na kuwa nao leo katika maisha yangu. Sitoacha kushukuru na nitaendelea kushukuru mara kwa mara. Bila yeye, leo nisingekuwa namfahamu Kelvin Kitaso, bila yeye nisingekuwa nikimfahamu Adabert Chenche, bila yeye nisingeweza kukutana wala kumfahamu Elioth Ushindi, na wengine wengi ambao kwa sehemu kubwa wameathiri maisha yangu na kunijenga kimaono zaidi.

JOAS ni kijana mhamasishaji, mwandishi na mfanyabiasha wa kitanzania anayefamika zaidi kwa jina la Jyb. Jyb ni kifupisho cha majina yake matatu; JOAS YUNUS BUYUNGU pia ni kifupi cha jina la kampuni yake maarufu ya ubunifu na ushonaji wa nguo na graphics design inayoenda kwa jina la JYB Modern Company aliyoianzisha na kuiasisi mwaka 2015 jijini Dar es salaam.

 Joas ameweza kufahamika na kupata umaarufu kupitia mitandao ya kijamii kama vile facebook, twitter, instagram, skype na whatsup na blogs mbalimbali za kiswahili kama www.kijanajithamini1.blogspot.com,  www.maishanamafanikio.blogspot.com.  Jina la Joas linazidi kujulikana na kuwa maarufu sio tu Tanzania, bali Afrika Mashariki na kati kwa sababu ya uwezo wake mkubwa wa kugusa, kuhamasisha na kubadilisha maisha ya watu wengi hasa vijana katika maeneo ya uongozi, biashara, imani, ujasiriamali na saikolojia.

            JOAS, WAZAZI NA NDUGU ZAKE.
Jackson Silvery akiwa na kitabu cha Inuka
JOAS ni mtoto wa nane kati ya watoto kumi wa Bwana Yunus Buyungu na Bi Yulini Yunus. Joas alizaliwa na kukulia katika familia ambayo lazima kila mtoto asali kabla ya kula, kulala na baada ya kuamka. Familia ya akina Joas, kwenda kanisani haikuwa hiari ilikuwa ni lazima. Mzee Yunusu Buyungu, baba yake mzazi wa Joas ni kiongozi na mshauri mwenye heshima kubwa sana kanisani. “Tangu mimi ni mdogo, mpaka nakua, baba yetu ni kiongozi kanisani. Nyumbani walikuwa wakija wachungaji na wainjilisti karibu kila jioni. Pia baba yangu mdogo alikuwa ndiye mchungaji mkuu kanisani. Tuliwajua viongozi na walimu wote kanisani na wao pia walitujua”.

Siku moja nimewahi kumuuliza Joas kwanini anabidii sana na hulka ya kufanya kazi kwa bidii? Katika maswali ambayo nimewahi kumuuliza hili ni swali ambalo lilionekana kumfurahisha, alicheka kidogo kisha akasema hivi, “Mama yangu alikuwa ni mtu wa mwisho kulala pia alikuwa ni wa kwanza kuamka. Kwa hiyo mama yangu alinifundisha kujituma sana na kuongeza bidii kila siku kwa kile ninachokifanya. Anaendelea kusema, siku zote tumekuwa tukiwapa nafasi sana baba zetu kwa sababu ni wanaume, ila kwangu mimi ni tofauti, mama alikuwa akinivutia sana, alijituma sana na mimi najituma sana kwa sababu ni kitu ambacho nilijifunza kwa mama yangu.

 Kumbuka kuwa, Joas ni mtoto wa tatu kutoka mwisho, ana ndugu tisa na mpaka leo amempoteza dada yake mmoja ambaye alishatengulia mbele ya haki na mimi natumia fursa hii kumuombea kwa Mungu, alale mahali pema peponi amina!. Joas ni miongoni mwa watu waliobahatika kuzaliwa katika familia kubwa, yenye watoto wengi. Nakumbuka siku ya uzinduzi wa hiki kitabu, nilikuwa nimekaa kiti cha kwanza mbele kabisa, nilikuwa na rafiki yangu Francis, nilishangaa kusikia Francis akiniambia hivi, “Edson, Joas ana ndugu wengi, halafu wanaoonekana wanajaliana!”. Hapo ilikuwa ni wakati wa kufungua kitabu ambapo kila mtu alipewa kipaza sauti na kujitambulisha na kununua kitabu.

Kama nilivyokwisha sema, Joas anazaliwa katika familia ya watoto kumi yeye akiwa ni mtoto wa nane kuzaliwa, tukimuondoa huyu ambaye alishatangulia mbele za haki, kuna Elias Yunus ambaye ni kitinda mimba, kuna Elianson Yunus, Devotha Yunus, Grace Yunus, Jackson Yunus, Anastastina Yunus, Elihud Yunus na Eric Yunus ambaye ni kifungua mimba.Na asilimia tisini ya hawa ndugu wote wa Joas wamesoma na ni wafanyakazi wengine wamejiajiri. Kwa kifupi Joas anatoka katika famila iliyo na mafanikio  makubwa kielimu, kiimani na kijamii pia. Mafanikio ya Joas kiroho, kifikra na kijamii ni picha halisi ya familia yake. 

            WALIMU NA ELIMU YAKE.

KITAALUMA, Joas ni mwanasayansi wa sayansi ya kompyuta. Amehitimu shahada ya sayansi ya kompyuta mwaka 2014 katika chuo kikuu cha Dar es salaamu. Akiwa Chuo aliweza kukutana na rafiki yake kipenzi bwana Kelvin Kitaso(ntamuongelea baadaye kidogo) pia maisha yake ya chuo yalikuwa ya kiimani sana na alipendelea kuwa katika vikundi vya dini. Huyu rafiki yake alikuwa kiongozi wa Casfeta Tayomi, kikundi cha dini kabla ya kuwa mchungaji msaidizi. Wakati huo Kelvin Kitaso alikuwa ni mwandishi tayari. Mbali na Kelvin Kitaso kuna kijana mwingine anayeenda kwa jina la Adabert Chenche, mwandishi wa vitabu kama vile Kwanini Ufeli? n.k.

Dada Magreth akiwa amejipatia kitabu cha Inuka
SIKU moja nilimuuliza, Joas, ni mhadhiri yupi aliyekuwa akikuhamasisha kipindi uko chuoni?, aliniambia kuwa wapo wengi, pia alidai kuwa anawapenda sana walimu wake wote wa chuo na anawashukuru kwa mchango walioutoa katika maisha yake kupelekea yeye kuwa Joas ambaye tuko tunamuongelea leo hii. Alisema kuwa, “Professor Koda, anastahili pongezi  nyingi zaidi”.

Kidato cha tano na cha sita, Joas alikuwa akisoma mchepuo wa PCM, Physics, Chemistry na Mathematics. Embu chukua sekunde thelathini kutafakari aina ya watu wanaochukua michepuo kama hii ya Joas, bila shaka utagundua ni watu wenye uwezo mkubwa sana darasani. Elimu yake ya kidato cha tano na cha sita aliichukua katika shule maarufu sana hapa Dar es salaamu, Pugu Sekondari School.Maisha yake hapo shuleni Pugu alimpenda sana Mwalimu Manyilizu. Alikuwa ni mwalimu wake wa Hesabu. Kidato cha kwanza na cha pili alisoma shule ya Kantalamba iliyoko Sumbawanga na alikuwa mwanafaunzi aliyependa kuwafundisha wanafunzi wenzake. Hakuwahi kuwa mbinafsi maisha yake yote. Wanafunzi wenzake walimpenda kwa sababu ya moyo wake wa kuwasaidia wenzake. Joas hajabadilika, mpaka leo ni mtu wa kujitahidi kuisaidia jamii kutoka hapo ilipo kwenda pale inapotamani kuwa. 

KWA upande wangu mimi, maisha yangu yote tangu nimefahamu kusoma na kuandika, nimekuwa msomaji wa vitabu vya aina zote. Sijisifii ila nilijua kuandika jina langu siku ya kwanza nilipoenda shule, hata kabla sijaanza shule nilipenda kalamu na karatas kuliko hata chakula. Nimeanza kusoma vitabu ambavyo siyo vya kujibia mtihani tangu niko vidudu, nimeanza kusoma hadithi za kwenye magazeti tangu mdogo sana. Namshukuru sana Mwalimu wangu tangu mtoto, Mwalimu Weston Yohana, maarufu kama Tesa. Alitambua kuwa nilikuwa napenda vitabu kwa hiyo muda wote alikuwa akinipa vitabu. Kwa muda wa miaka mingi, waandishi wengi wamekuwa wakimwambia msomaji wao kuwa INAWEZEKANA lakini hawasemi INAWEZEKANA VIPI.
Joas sio mtu wa kukuambia kuwa inawezekana tu, bali pia ni mtu wa kukuambia inawezekana vipi. Siku zote amekuwa sio mhamasishaji tu bali ni mwalimu na mkufunzi wa mafanikio anayetoa njia na mbinu zilizo rahisi kufikia ndoto na malengo yako. Kama umewahi kukaa na Joas au hata kuzungumza naye utakuwa ni shahidi wa hili ambalo nataka niliseme, Joas ni mzuri sana katika kuzungumza Kiigereza. Hatusemi kwamba kujua au kutokujua kingereza ni maada ya kujadiliana, hapana!, hata kama ni mada ya kujadiliana, kwani hatujui kuwa Tanzania ni nchi inayoongoza kuwa na wahitimu wasioweza hata kujieleza kwa kingereza?. Tuachane na hayo. Nachomaanisha hapa ni kwamba, Joas hakusoma mchepuo wa Kiingereza wala Historia, mara nyingi tunaamini kuwa wanafunzi wa masomo ya sanaa huwa ndiyo wazuri katika kuongea kiingereza na huo ndio ukweli na mimi ninayeongea hivi kitaaluma ni Mwalimu kwa hiyo na tajiriba ya kutosha katika hili eneo. 

NILIWAHI kumuuliza, Joas, ulijifunza lini na wapi kuzungumza Kiingereza fasaha kiasa hicho?. “Mwalimu wangu wa shule ya msingi alikuwa vizuri sana. Alikuwa akitufundisha kwa namna ambayo lazima utajua pia utaelewa. Nilikuwa nikimpenda sana Mwalimu wangu wa kiingereza, Mwalimu Ezekiel Marius alijua sana kufundisha kingereza kwa ustadi mkubwa.
    MARAFIKI NA WAHAMASISHAJI WA JOAS

ZIG ZIGLAR, aliwahi kusema hivi, “ukiwa karibu ya watu watano wanaojiamini jiandae kuwa mtu wa sita kujiamini, ukiwa karibu ya watu watano wenye busara, jiandae kuwa mtu wa sita kwa busara, ukiwa karibu ya watu watano wenye pesa jiandae kuwa mtu wa sita kwa pesa na ukiwa karibu ya wapumbavu watano jiandae kuwa………………… Kwa lugha nyingine tunasema hivi, sisi ni wastani wa  watu sita tulioishi na kukaa nao kwa kipindi kirefu cha maisha yetu. Waganda wanasema hivi, “nioneshe rafiki zako nitakuambia wewe ni nani”(show me your friends, I shall tell you who you are)

Jamaa yangu aliwahi kuniambia hivi ukiwa karibu ya wezi watatu, jiandae kuwa mwizi wa nne. Maneno haya yananikumbusha  baadhi ya vipindi nilivyowahi kupitia shuleni. Kuna wakati nilikuwa nikionekana katikati ya wanafunzi wakorofi na watukutu walioshindikana hata kwa walimu na kwa wazazi wao. Siku moja mwalimu wangu wa taaluma, Mwalimu Meshaki aliniita ofisini kwake akaniambia maneno ambayo sijawahi kuyasahau mpaka leo. “Kashindi, angalia vizuri hao rafiki zako. Sisi tunakupenda!, hatutaki uwe kama wao. Wewe una akili. Kashindi ,usipoangalia vizuri unaenda kuharibikiwa. Wale rafiki zako sio wazuri, tabia zao sio nzuri, hawapendi shule”. Nilitaka nimuulize swali, lakini nilipoangalia macho yake nikagundua alikuwa kachukia pia aliongea kwa masikitiko sana na macho yake yalikuwa kama yana machozi kwa mbali. Baada ya hapo nilimshukuru kwa ushauri kisha nikaondoka.

ILIKUWA ni mwanzoni mwa mwaka wa 2016, ambapo Joas alinipigia simu na kuniambia kwamba kuna mtu anaitwa Kelvin Kitaso anahitaji mtu wa kumsambazia vitabu na kunielekeza kuwa kwa kila kitabu unachouza kuna asilimia fulani kwa ajili yako. Nilifurahi sana na baadaye kidogo Kelvin Kitaso alinipigia simu na kuniambia kuwa namba yangu alipewa na bwana Joas na kunieleza kila kitu na tukapanga siku ya kuonana huku tukikubaliana kwamba atakuja DUCE(Chuo nilichokuwa nasoma kipindi hicho) na vitabu ili niwe naviuza chuoni na sehemu zingine. Nakumbuka alikuja siku ya jumapili akiwa ameambatana na binti fulani ambaye sikuwa nikimfahamu, tuliongea ingawa sio kwa muda mrefu ila alionekana kusikitishwa na vijana kutosoma vitabu vya maendeleo binafsi. Kabla ya hapo nilianza kumsikia Kelvin Kitaso kupitia kundi la KIJANA JITHAMINI.
JOAS nimemfahamu muda mrefu sana, zaidi ya miaka kumi, Joas hakuwa mwandishi zaidi tu, Joas alipenda kusoma vitabu. Kuna kipindi nilipotezana naye nikawa siwasiliani naye kwa kipindi cha zaidi ya miaka mitatu na nadhani ilikuwa ni kwa sababu ya shule. Mimi nimeanza kuandika makala za hip hop, falsafa na masuala ya harakati facebook. Kuna siku nilibahatika kumuona Joas facebook ikabidi nimuombe urafiki. Nilianza kuona akiandika masuala ya kufikirisha na yenye changamoto huku akitumia falsafa za akina Jim Rohn na Kop Meyer. Sikushangaa sana kwa sababu Joas alisoma sana vitabu tangu zamani. Baadaye kidogo nikaanza kutoa maoni na kumuuliza maswali ya yaliyobeba changamoto za makala zake. Hazikupita siku nyingi Joas alinitumia ujumbe na tukaanza kuwasiliana tena na kurudisha ukaribu wetu kama ilivyokuwa zamani.

 Aliniuliza malengo yangu nini nikamuambia. Nachoshukuru tu Joas anapenda sana watu wafanikiwe na nadhani hii ndiyo asili yake.
Hazikupita siku nyingi Joas aliniunganisha kwenye group la KIJANA JITHAMINI ambapo nilikuja kuanza kuwasikia akina Adabert Chenche, Ushindi Elioth na wengine wengi ambao ni waandishi. Joas alianza kunichukulia kama mwandishi, nadhani ni baada ya kujua maono na ndoto zangu, pia kipindi tunarudisha mawasiliano nilikuwa naandika kitabu kinachohusu masuala ya hip hop ila kwa bahati mbaya hakijatoka mpaka leo ila tunaamini kitatoka. Mungu atatusaidia.
BAADA ya muda mfupi tulipata wazo la kuanzisha magazine(Kijigazeti) la masuala ya uhamasishaji na nakumbuka hilo wazo lilitufanya kukutana wote mimi, Mihayo, Joas, Kitaso, Adabert na Laban . Kwa mara ya kwanza nikakutana na Adabert, Mihayo na wengine. Hawa wote kwa pamoja ni waandishi, jiulize Joas angekuwa nani?.  Lazima Joas angekuwa mwandishi. Kwa hiyo Joas alijikuta yuko katikati ya waandishi akajikuta na yeye amekuwa mwandishi ukijumlisha na tabia yake ya kusoma vitabu.
JOAS ni kijana anayepambana usiku na mchana kuathiri kizazi cha sasa na cha kesho na kuleta matokeo makubwa yaliyo CHANYA katika maisha ya watu wengi zaidi hasa vijana. Kitaaluma Joas ni mwanasayansi  wa  sayansi ya  kompyuta, mwasisi wa kundi la kundi la KIJANA JITHAMINI, kundi linaloendesha shughuli zake kupitia mitandao kama whatsApp, facebook na blogs.
 Kijana Jithamini ni kundi la vijana walioamua kutumia muda wao kuelimishana, kuhamasishana na kushirikiana katika shughuli mbalimbali za maendeleo na mafanikio. Vijana wanaounda Kijana Jithamini wamekuwa mfano bora na hamasa kubwa sana kwa vijana wengi wa kitanzania hasa kwa maono na mitazamo na ndoto kubwa zilizomo vichwani na mioyoni mwao. Kundi la Kijana Jithamini linaundwa na vijana walioamua kuacha kulalamika na kuchukua hatua madhubuti za kupambana na kupiga vita ujinga, maradhi na umaskini nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Miongoni mwa vijana maarufu wanounda kundi hilo ni; Mwandishi wa kitabu bora cha wanafunzi vyuoni cha Getting Prepared For Post University Life ambaye pia ni Mwasisi na Rais wa taaisi ya kijamii ya RFGM na Mkurugenzi wa kampuni kubwa ya uchapishaji wa vitabu hapa nchini Gracious Printing Press, mhamasishaji  ndugu Kelvin Kitaso. Adabert Cheche, mwanzilishi wa taaisi ya VIPAWA LINK, mhamasishaji na mwandishi wa vitabu kama Kwanini Ufeli, Manukato ya Mafanikio. Ushindi Elioth  Mwandishi wa kitabu cha “A walk to financial Freedom “ na Kitabu cha “Urejesho wa Ibada ya Mugu wa kweli”.

Mbali na kuwakutanisha na kuwanganisha pamoja vijana walio na maono na mitazamo chanya, Joas ni miongoni mwa waasisi wa taasisi isiyo ya kiserikali  iliyoko Tabata jijini Dar es salaam inayojihusisha na masuala ya Afya ya Mama na Mtoto inayojulikana kwa jina la LULU NZURI FOUNDATION.
Joas pia ni mwandishi wa makala maarufu sana ya kuhamasisha na kubadalili mitazamo ya haiwezekani kuwa inawezekana, MORNING RISE UP. Haya ni makala yanayoandikwa kupitia mitandao ya kijamii na kugusa maisha ya watu wengi hasa kwa ujumbe muhimu na hamasa kubwa inayobebwa kwenye haya makala.
JOAS, ni watu gani ambao wamekuhamasisha na kukufanya ufikie hatua ya kuanza kufundisha na kuhamasisha watu wengine?. “Ni watu wengi. Kwanza kabisa, nahamasishwa na marafiki zangu, akina Kelvin Kitaso, Adabert Chenche, Daniel Rwihula,Widom Misana ,Adam Ngamange ,Nicholous Mwakyonde(Zingo) , Patrick Roman ,Amina Sanga ,Subira Mlaga ,Rehema Robert , Fred Mwahelende ,Robson Sisyan ,Seth Jacob, Ushindi Elioth , Lendian Bigoli ,Jacob Mushi(mwandishi wa kitabu cha Siri saba za kuwa hai Leo), lazaRo Samwel(mwandishi wa kitabu cha Siri Tatu za Maisha) na wengine wengi. Pia kuna watu kama Jim Rohn, Robert Kiyosaki, Eric Shigongo, Dr Moyles, na Nelson Mandela, Napoleon. Najifunza vitu vingi sana kutokwa kwa hawa watu.

HISTORIA ya Joas bado ni ndefu sana na inaishi na bado inakua. Inapendeza sana kusoma historia huku na wewe ukiwa unaweka historia.
Usihitaji kukubalika, hitaji kukumbukwa.
                       
Ahsante sana. Naitwa Kashindi Edson hongera kwa kupata nakala ya INUKA 

 




NITAMILIKI BIASHARA YANGU SEHEMU YA SITA



                             NAMNA YA KUPATA MTAJI


Watu wengi wanatamani kuanza biashara lakini wanasingizia kuwa hawana mitaji .Leo Jyb atakueleza mitaji uliyonayo ambayo pengine ulikuwa hufahamu kama unayo na umebaki ukilalamika;


1. Kutumia akili yako (your mind) Kuna watu watapigwa na butwaa lakini ukweli mtaji wa kwanza ulionao ni akili ambayo Mungu alikupa buree kabisa .Huu pengine ndio mtaji mkubwa kuliko mitaji yote duniani bahati mbaya unaweza kuwa ulikuwa hujafahamu na hata mwalimu wako wa chuo kikuu hakukufundisha.

Akili yako ndiyo suluhisho la jambo lolote .Akili yako ndiyo yenye uwezo wa kuzalisha mawazo yenye kuleta mtaji .Ni lazima ili upate mtaji uitumie akili yako vizuri kuwaza kwa kina jinsi ya kupata mtaji vinginevyo utabaki unalalamika.

Kwa mfano kuna mtu anatafuta mtaji wa laki tano wakati huo anamiliki simu ya laki sita, American boot ya laki moja , Nguo za kutosha ,boda boda kila siku n,k .Mtu huyu kakosa mtaji au kakosa akili?.Kwanini asianze kuuza alivyo navyo na kupunguza matumizi apate mtaji?


  2. Kutumia kipaji chako (your talent )
Kipaji chako ni mtaji mkubwa sana ambao Mungu amekupa na kwa bahati mbaya watu huwa hatutaki kujua tuna vipaji gani na hata kama tunajua hatujui kuvitumia na bado tunaendelea kulalamika na kuilalamikia serikali kuwa hatuna mitaji .

Nguvu ya mbegu iko ndani ya mbegu yenyewe hata nguvu,uwezo ,vipawa ,vipaji viko ndani yako lakini umeshindwa kuvitumia na maisha yako yanaonesha hayana mwelekeo kabisa .

Angalia watu ambao shughuli kubwa ni kucheza kwenye maharusi (dancers) na baada ya harusi watu hawa hulipwa kwa sababu ya vipaji vyao na ukweli wanatangeneza hela nyingi sana .Wewe una kipaji gani kikupe fedha??

Angalia wachezaji wa mpira ambao ndio wanaoongoza kwa kulipwa fedha nyingi duniani ni kwa sababu wametumia vipaji vyao walivyopewa na Mungu na vinawalipa sana na chenji inabaki .Wewe ni shahidi kuwa Ronaldo ,Leonal Messi wanalipwa hela nyingi sana .Lakini hapa kwetu Mbwana Sammata ambaye elimu yake siyo kama yako analipwa hela nyingi kwa sababu ya kipaji alichonacho.

Rose Muhando hata sifahamu ana elimu gani lakini jambo ninalofahamu ni kuwa ni mwimbaji maarufu na hapatikani kirahisi bila hela ya kutosha .Nini siri ya Rose Muhando? .Siri ni kuwa aligundua nguvu/uwezo/kipaji chake na akakitumia na sasa kinamlipa .Vipi kuhusu MASANJA?.

Ni lazima ujue una kipaji gani na kukutumia kwa viwango vikubwa na vya tofauti ili kianze kukulipa vinginevyo utabaki kama ulivyo.


     3.Kutumia Ujuzi wako (your skills)
Ujuzi wako ni mtaji mkubwa ulionao .Ni lazima utumie ujuzi ulio nao ili uanze kuzalisha fedha kwa kutumia ujuzi wako vinginevyo utabaki hapo ukilalamika wakati wengine wanatumia ujuzi wao kupiga hatua .

Gerad Saul ni rafiki yangu ambaye alihitimu chuo kikuu IFM  na  shahada ya sayansi ya Bima na udhibiti Majanga (Insurance & Risk Management mwaka 2013 na hakuwa na mtaji lakini akajua kuwa alikuwa na ujuzi wa kushona nguo ujuzi ambao aliupata kwa baba yake .Gerad baada ya kumaliza chuo alifungua sehemu yake ya kushona kwa kuwa mwanzoni alianza kushona kwa watu akapata mtaji na sasa anamiliki kiwanda chake kidogo cha nguo nay eye anashona na shahada yake kichwani

lazima ufahamu kuwa kama una ujuzi, huo ni mtaji wako kabisa hivyo utumia upate fedha kuliko kubaki unalalamika.


4. Kutumia Watu wanaokuzunguka(your network ) Watu wanaokuzunguka ni mtaji kwako ambao Mungu amekupa kabisa lakini bado huna uwezo wa kuwafanya kuwa chanzo cha mtaji wako na umebaki ukilalamika kwa kuwa umekosa maarifa ya kutumia watu wanaokuzunguka.

Watu ndio wenye fedha na kumbe kama watu ndio wenye fedha na wewe umezungukwa na watu hao kwanini unasema umekosa mtaji ?.Shida huna maarifa ya kutosha na wala siyo ukosefu wa mtaji .

Kaa chini angalia watu waliokuzunguka ni watu wa namna gani .Fikiria wazo ambalo linaweza likamfanya huyo ndugu yako atoe fedha kwa ajili yako.Mara nyingi hata ndugu yako anaweza asikupe fedha kama huna bidhaa yoyote ya kumuizia .Ni lazima kuwa na kitu fulani chenye thamani ndipo mtu akupe fedha mbali na hapo huwezi kupata chochote kutoka kwa watu waliokuzunguka .

Kwa mfano kama una mtandao wa watu 1000 wanaokufahamu na ukawa  na wazo zuri lenye mashiko na ukawashawishi watu hawa wakuchangie kiasi cha shillingi elfu kumi tu (10,000/=)  maana yake utakuwa na uwezo wa kukusanya sh milioni kumi ambao ni mtaji mkubwa sana .

Unaweza pia  kutafuta watu ambao wewe unawaamini mkaamua kuchangiana fedha kwa mzunguko .Kwa mfano ukipata watu sita ambao mnaweza kuchangiana shilling laki moja tayari utakuwa na shilling laki sita fedha ambayo unaweza kuitumia kufanya jambo fulani lenye tija .

   5. Kuweka Akiba(Saving )

Siku moja nikasikia mtu ambaye analalamika kuwa hana mtaji wa laki tatu .Mtu huyu kama alikosa mtaji wa laki tatu maana yake kwa siku hakuwa na uwezo wa kuweka shillingi elfu moja kama akiba maana kama ukiweka kila mwisho wa mwaka na alikuwa mfanyakazi wa muda mrefu nilistuka sana siku sh 1000 kwa siku miatatu sitinI na sita kwa mwaka inakuwa laki tatu na sitini na kama unaweka 2000 unapata laki saba na kama unaweka elfu tatu kila siku kwa mwaka utapata milioni moja.

Nilivyopiga mahesabu haya niligundua kuwa tunapoteza hela nyingi sana na tumekuwa na kasumba ya kudharau hela ndogo na tumebaki tukilalamika .2017 amua kuweka nidhamu ya fedha ili uanzishe biashara yako kabla mwaka haujaisha .Ukweli tumekuwa tukipata fedha lakini tumeshindwa kuzitumia vyema maana hatuna mipango hata kama majukumu tunayo mengi .

 6. Kubadilisha unavyomiliki kwenda kwenye fedha(converting things into money )

Moja ya namna ya kupata mtaji ni pamoja na kuuza ulivyo navyo  ili upate fedha za kukusaidia kuanzisha biashara .Kwa mfano kama una simu ya laki tatu na nusu na unatafuta mtaji wa sh laki mbili na nusu kwanini usiuze simu yako hiyo ufanye biashara ili baadae ukianza kupata faida uweze kununua simu nyingine.

Kuna vitu vingi tunavyo vya anasa ambavyo tunatumia pesa nyingi kuvinunua wakati fedha hizo ndizo zingetusaidia kupata mtaji wa kuanzia kwenye biashara zetu.

Joas